Loading...

Impact Story

Naitwa Angel Renatus, nina miaka 12, muhitimu wa shule ya msingi Pendo, iliyopo wilaya ya Ilemela, mkoa wa Mwanza. Mimi ni mtoto wa kwanza katika familia yetu ya watoto watatu.
Nilishiriki mashindano ya Msichana Tai yanayoendeshwa na shirika la MsichanaTai, ambayo yanawapa wasichana na wavulana fursa ya kujiamini na kupigania ndoto zao. Mashindano haya yalihusu ubunifu wa kusoma kitabu cha ‘Msichana ni Tai, Sio Kuku’, kinachozungumzia maisha ya Malkia wa Kiafrika waliotawala tangu karne ya 14.
Miongoni mwa Malkia waliotajwa, Malkia Amina wa Zazzau kutoka Nigeria alinivutia zaidi. Aliongoza jeshi la wanaume 20,000 na kupigana vita kwa miaka 34, huku akitengeneza ngome na vifaa vya ulinzi kwa askari wake. Ujasiri wake ulinifunza kuwa hakuna changamoto isiyoweza kutatuliwa. Kitabu hiki kilinifungua macho sikujua kuwa wanawake waliongoza dola kubwa barani Afrika kwa ujasiri na uthubutu.
Katika mashindano hayo, nilishinda mara tatu kwenye vipengele tofauti. Kwanza, nilishirikiana na marafiki zangu kuimba wimbo uliobeba ujumbe wa kitabu hiki. Pili, nilibuni michoro ya batiki, ubunifu wangu ukapata ushindi. Mwisho, nilishiriki kwa njia ya mashairi na nikafanikiwa kushinda. Mafanikio haya yalinipa motisha kubwa na kuniimarisha zaidi.
Kupitia mashindano haya, nimeweza kuwa jasiri zaidi. Niliwania nafasi ya uongozi shuleni na nikachaguliwa kuwa dada mkuu. Pia nimeendeleza kipaji changu cha ubunifu kwa kutengeneza michoro ya batiki na kuwafundisha rafiki zangu, jambo ambalo limenipa furaha na kuniwezesha kujipatia kipato kidogo.
Mama yangu ni nguzo yangu; daima ananihamasisha na kujivunia mafanikio yangu. Ndoto yangu kubwa ni kutaka kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kama Malkia waliotajwa kwenye kitabu cha ‘Msichana ni Tai, Sio Kuku’ waliweza kutawala na kuleta mabadiliko, kwanini mimi nishindwe?
Ninashukuru Shirika la MsichanaTai kwa kunipa mwanga kupitia kitabu hicho, ambacho kimenijenga na kuniandaa kwa safari yangu ya kufikia ndoto kubwa.

More Impact Stories

Neema Reuben
Neema Reuben

Neema Reuben alikabiliana na changamoto, akapata ujuzi wa ushonaji na kujenga ujasiri. Anataka kusaidia wasichana wengine.

Learn More
Eliana
Eliana

Eliana binti jasiri, alikabiliana na changamoto, akawa mtaalamu wa urembo Kayenze, anasaidia wasichana.

Learn More
Maria Joseph
Maria Joseph

Maria Joseph, msichana shujaa, anajivunia ngozi yake ya giza, anafikia malengo yake.

Learn More
Angel Damas
Angel Damas

Angel Renatus, msichana mwenye umri wa miaka 12, anashiriki mashindano ya Msichana Tai na kushinda. Kwa kuhamasishwa na Malkia Amina wa Zazzau, anakuza ujasiri na ubunifu wake. Je, atafikia ndoto yake ya kuwa Rais? Soma zaidi ili ujifunze kuhusu safari yake ya kuvutia!

Learn More

Eagle Movement for Adolescent Girls!

Join the movement and be part of the change that's transforming lives and breaking barriers.

Join The Movement Today