Mafunzo yameniinua sasa nasomesha mtoto wangu, napambana kumtoa mama kwenye nyumba inayovuja’.
Neema Samson (23) Mkazi wa Buswelu wilayani Ilemela mkoani Mwanza, Mtoto wa tatu kati ya watoto sita ambao wanalelewa na mama yao.
Neema anasema kutokana na changamoto za maisha alipata ujauzito akiwa na umri mdogo hatua iliyomfanya apitie mazingira magumu na kuishi huku akitegemea mama yake ambayo hana chazo chochote cha kumuingizia kipato.
“Sisi hatuna baba tayari ametangulia mbele za haki lakini pia maisha yetu yalikuwa magumu zaidi hivyo ikabidi nianze kujishughulisha na kuuza makongoro na mihogo ya kukaanga. Siku zote ng’ombe wa masikini wanasema hazai, hata fedha niliyoipata kwenye shughuli hiyo ilipeperushwa na changamoto za hapa na pale na hata hivyo haikuwa n auwezo wa kukimu mahitaji yetu,”anasema Neema
Aidha anasema alianza kuona mwanga katika maisha yake mwezi wa tano 2025 alipopata fursa ya ufadhili wa mafunzo ya upishi ‘hotel manegment’ pale Pizelia uliotolewa na Shirika la Msichana Tai na kumuwezesha kupata ujuzi katika fani hiyo ya mapishi.
“Kuanzia hapo si hali yangu tu ya maisha iliyobadilika bali pia na nyumbani tulianza kupata uhakika wa chakula na pia nimefanikiwa kupeleka mtoto wangu menye umri wa miaka mitano katika shule na nina uwezo wa kumlipia Ada ya Sh.100,000 kwa mwezi.
Anasema baada ya mafunzo hayo alipata kazi ambayo kwa sasa inamuwezesha kuingiza zaidi Sh.7000 kwa siku sawa na Sh.210,000 hatua inayomsaidia kuendelea kukidhi mahitaji yake binafsi, mtoto pamoja na mama yake mzazi.
“Kwasasa mambo yanayoniumiza zaidi ni pamoja na nyumba yetu ambayo bati zake zimeegeshwa kwa juu hivyo naendelea kupambana niezeka nyumba hii ya mama ili aache kuishi sehemu inayovuja hasa wakati wa mvua ambako maji yanaingia ndani ya nyumba yetu hivyo huu ni miongoni mwa mipango yangu,”anasema Neema.
Aidha anasema katika ndoto zake anatamani kufika mbali zaidi ikiwa ni pamoja na kuanzisha biashara ya chakula kubwa, kuhakiki anajenga vema nyumba anakoishi mama yake.
“Niendelee kuushukuru uongozi wa shirika la Msichana Tai na kuwaomba waendelee kuwawezesha mabinti ili wafike mbalimbali kupitia kupitia fani mbalimbali, bila kujali changamoto wanazozipitia ili nao waliopoteza muelekeo wapate pa kuanzia,” anasema Neema.
Aidha Neema anawakumbusha mabinti kutokuacha fursa waionapo, wajitose na kuhakikisha wanafanya liwezekanalo ili kuweza kutumia ujuzi katika kujiinua kiuchumi na kuondoka na utegemezi katika jamii.
Neema Reuben alikabiliana na changamoto, akapata ujuzi wa ushonaji na kujenga ujasiri. Anataka kusaidia wasichana wengine.
Learn More
Eliana binti jasiri, alikabiliana na changamoto, akawa mtaalamu wa urembo Kayenze, anasaidia wasichana.
Learn More
Maria Joseph, msichana shujaa, anajivunia ngozi yake ya giza, anafikia malengo yake.
Learn More
Angel Renatus, msichana mwenye umri wa miaka 12, anashiriki mashindano ya Msichana Tai na kushinda. Kwa kuhamasishwa na Malkia Amina wa Zazzau, anakuza ujasiri na ubunifu wake. Je, atafikia ndoto yake ya kuwa Rais? Soma zaidi ili ujifunze kuhusu safari yake ya kuvutia!
Learn More